Kiungo wa Azam FC, Yannick Bangala, ameumia nyama za paja katika mechi na hajulikani muda wa kupona
Kiungo Mkongo wa timu ya Azam FC, Yannick Bangala, ameshanika nyama za paja na bado haijajulikana atakuwa nje ya uwanja kwa muda gani.
Bangala ambaye alisajiliwa na timu hiyo akitokea kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga, amepata tatizo hilo wakati wa mechi yao dhidi ya Dodoma Jiji iliyomalizika kwa suluhu.
22:00 - 04.10.2023
KANDANDA Robertinho aifungia kazi Prisons
Robertinho anakumbuka Juni 26, mwaka jana wakiwa kwenye uwanja huo walikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa maafande hao wa Magereza.
Kiungo huyo anaungana na wachezaji wengine kama straika Prince Dube na kiungo, Yahya Zayd katika benchi la majeruhi.
Taarifa ya Azam FC imeeleza kwamba baada ya mechi hiyo, Bangala alirejea Dar es Salaam kwa vipimo zaidi, wakati timu ikienda jiji Tanga kwa ajili ya mchezo wa Ijumaa dhidi ya Coastal Union.
13:11 - 02.10.2023
KANDANDA Azam FC yapata pigo, nyota wawili 'out'
Wachezaji hao wanaendelea na programu ya kutibu majeraha yao chini ya uangalizi wa Mtaalamu wa tiba za viungo wa timu, Joao Rodrigues.
“Baada ya vipimo ndiyo itajulikana ukubwa wa tatizo na muda wa matibabu hadi kupona,” imesema taarifa ya Azam FC.
Katika mchezo huo uliopigwa Dodoma, Bangala alikuwa mhimili mkubwa kwa Azam katika eneo la kiungo akishirikiana na Feisal Salum na Sospeter Bajana na kuwapa wakati mgumu wapinzani wao.
12:30 - 02.10.2023
KANDANDA Tanzania yaingiza timu mbili makundi CAFCL
Yanga jana imefuzu hatua hiyo kwa mara ya kwanza ikipita miaka 25 baada ya kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 3-0 dhidi ya Al-Merreikh ya Sudan.
Kutoka kwake ambapo nafasi ilichukuliwa na Ayoub Lyanga kuliifanya timu yake kuwa na wakati mgumu kwa Dodoma Jiji kuanza kuliandama lango lao.
Hata hivyo, Kocha wa timu hiyo, Youssouph Dabo, akizungumzia kuumia kwa Bangala, amesema ni pigo kwa timu yake lakini wataendelea kuboresha safu ya kiungo kwani ana wachezaji wenye uwezo mkubwa.