Hiyo huenda ikasaidia kupunguza malalamiko yanayokuwa yakitolewa kwa waamuzi wakidaiwa kushindwa kutafsiri sheria 17 za soka
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limeipa nchi ya Tanzania video za usaidizi wa marefa (VAR) ambazo zitafungwa nchini kwenye viwanja vyenye ubora.
Hayo yamethibitishwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia wakati akitoa hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo uliofanyika mkoani Iringa.
09:15 - 16.12.2023
LIGI KUU Gamondi ataka nyota wake kujituma ili wacheze
Kocha huyo wa Yanga ametoa kauli hiyo baada ya wachambuzi wa soka nchini Tanzania kushauri awe anabadili kikosi chake
Karia amesema tayari wataalamu wa kufunga vifaa hivyo na kutoa mafunzo wameshafika nchini tangu jana na kazi itaanza hivi karibuni.
Aidha amesema kupewa vifaa hivyo ni kutokana na ushirikiano mzuri kati yao na CAF.
22:00 - 15.12.2023
KANDANDA Benchikha apata ushindi wa kwanza Ligi Kuu
Hiyo ni mechi yake ya tatu tangu apewe mikoba hiyo huku akiiongoza timu ya Simba SC katika mechi mbili za kimataifa bila ushindi
"Hivi karibuni tutaanza zoezi la kufunga VAR, wataalamu wameshafika tangu jana," amesema.
Zoezi hilo linatarajia kufanyika katika viwanja ambavyo vimekizi vigezo vya CAF ikiwemo Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.
19:00 - 14.12.2023
LIGI KUU CEO wa Yanga SC atamba kutetea mataji yao
Bosi huyo ametoa kauli hiyo wakati timu yake ikijiandaa na mechi zaidi ya tatu kabla ya mwaka mpya kuingia
Tanzania ikifanikiwa kufunga VAR itaungana na nchi zingine za Afrika kama Misri, Algeria na Morocco ambazo tayari zinatumia kifaa hicho.