David Ouma arithi mikoba ya Zahera Coastal Union

KANDANDA David Ouma arithi mikoba ya Zahera Coastal Union

Abigael Wafula • Na Zahoro Mlanzi • 21:00 - 09.11.2023

Ni kocha anayeheshimika ndani ya Kenya na amefanya kazi kwa muda mrefu na kikosi cha Sofapaka na katika nafasi tofauti ikiwemo ya Ukurugenzi wa Ufundi.

Klabu ya Coastal Union ya mkoani Tanga, imemtambulisha David Ouma raia wa Kenya kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho.

Ouma anaziba nafasi iliyoachwa wazi na Kocha Mkongo, Mwinyi Zahera ambaye alisimamishwa kazi mwezi uliopita.

Kocha huyo mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 15, amepita katika Kituo cha Michezo cha Ajax cha nchini Uholanzi, ana Leseni ya UEFA na Leseni A ya CAF na pia amewahi kupata mafanikio ndani ya Klabu ya Sofapaka na timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars'.

Ouma ni kocha anayeheshimika sana ndani ya Kenya na amefanya kazi kwa muda mrefu na kikosi cha Sofapaka akiwa ameitumikia katika nafasi tofauti ikiwemo nafasi ya Mkurugenzi wa Ufundi.

Anakuja kujiunga na kikosi cha Coastal Union ambacho kina mwendo ambao sio wa kuridhisha kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Kwasasa kikosi cha Coastal Union 'Wagosi wakaya', kilikuwa chini ya Kocha Fikiri Elias ambaye alishika nafasi hiyo kwa muda.

Coastal Union kwasasa wapo nafasi ya 13 kweye msimo wa ligi hiyo wakiwa na alama 7 baada ya kushuka dimbani mara 9.

Ouma atalazimika kuanza maandalizi yake mapema kwenye kipindi hiki cha mapumziko ya timu za taifa na mara baada ya ligi kurejea mechi yake ya kwanza itakuwa ni dhidi ya Singida Fountaon Gate ugenini kwenye Uwanja wa Liti.

Tags: