Kauli hiyo imekujaa baada ya kuiongoza timu hiyo kushinda mechi mbili na sare moja
Kocha wa timu ya Yanga SC, Miguel Gamondi, amesema kwasasa kitu muhimu kwake ni alama tatu katika kila mchezo.
Hayo amesema mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi Kuu Bara ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mashujaa FC katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
16:20 - 08.02.2024
KANDANDA Yanga SC yazindua kadi ya uanachama yenye thamani ya sh. milioni 1
Kadi hiyo itamnufaisha mwanachama katika masuala mbalimbali zikiwemo huduma za kijamii na kibenki
Katika mchezo huo, iliwalazimu Yanga kusubiri tena hadi dakika za mwishoni ili kufunga bao la ushindi kupitia kwa kiungo wao, Mudathir Yahaya.
Mara baada ya mchezo huo, Gamondi amesema timu yake kwasasa haichezi kama alivyotarajia lakini kitu muhimu kwake ni kuvuna alama tatu.
10:04 - 09.02.2024
KANDANDA Simba SC, Azam FC ni mechi ya kisasi leo CCM Kirumba
Ni timu ambazo zimekuwa zikifanya vizuri katika Ligi Kuu Bara, hivyo mchezo huo utavuta hisia za mashabiki wengi
"Kwasasa hatupo katika hali nzuri ya kiushindani kama tulivyokuwa awali, hata hivyo muhimu zaidi tunavuna alama tatu," amesema.
Tangu kurejea kwa ligi hiyo, Yanga imecheza mechi tatu ambapo walianza kwa kulazimishwa suluhu na Kagera Sugar ugenini.
05:30 - 08.02.2024
KANDANDA Nyota 3 Yanga waongeza nguvu kuivaa Mashujaa FC
Wachezaji hao walikosekana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kucheza michuano ya AFCON
Mara baada ya mchezo huo, wakacheza mechi mbili dhidi ya Dodoma Jiji na Mashujaa ambapo mechi zote hizo walipata mabao ya ushindi kwenye dakika tano za mwisho.
Yanga sasa inajiandaa kwenda kukabiliana na Tanzania Prisons ya mkoani Mbeya mechi ambayo itachezwa kesho Uwanja wa Sokoine.