Tumecheza vizuri lakini wapinzani wetu walikuwa bora na hasa walituzidi katika uzoefu
Licha ya kupoteza kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Mamelodi Sundowns Ladies kwa 2-0, Kocha wa timu ya JKT Queens, Ester Chabruma, bado ana imani na kikosi chake ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa Wanawake.
Katika mchezo huo, ambao ulichezwa usiku wa kuamkia Jumatatu nchini Ivory Coast, JKT Queens walikubali kichapo hicho huku mabao ya Mamelodi yakifungwa na Lebogang Ramalepe na Refilwe Tholakele.
08:31 - 06.11.2023
KANDANDA Dkt. Samia aipa 'tano' Yanga kuifunga Simba 5-1
Upinzani wenu wa jadi wa zaidi ya miaka 85 sasa ni sehemu muhimu ya burudani ya Watanzania
Mara baada ya mchezo huo, Kocha Chabruma, amezungumza kwa simu kutoka Ivory Coast, akisema wamecheza vizuri lakini wapinzani wao walikuwa bora na hasa waliwazidi katika uzoefu.
Hata hivyo amekiri nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo bado wanayo kwani wana michezo miwili ambayo watajipanga kufanya vizuri.
"Kikosi chetu hakijacheza vibaya ila ni makosa tu ndio yaliyofanya tufungwe, wapinzani wetu ni bora na wana uzoefu mkubwa tofauti na sisi," amesema.
20:00 - 05.11.2023
KANDANDA Yanga yaipiga Simba 5G Ligi Kuu
Ushindi huo, unaifanya Yanga kulipa kisasi cha miaka 10 iliyopita kwani mwaka 2013 nao walifungwa mabao 5-0 na Simba
'Nafasi bado ipo kwa hivyo ni jukumu letu kufanyia kazi mapungufu yetu ili tuweze kurekebisha katika mechi zijazo," amesema.
JKT watashuka tena uwanjani Jumatano kwa ajili ya mchezo wa pili ambao watacheza dhidi ya wenyeji Athletico Abidjan mchezo utakaopigwa saa 11.
17:30 - 05.11.2023
KANDANDA Moalin: Siwezi kurudi Azam FC
Kocha huyo amewahi kuifundisha Azam kabla ya kuvunjiwa mkataba na nafasi yake kuchukuliwa na Kali Ongala
Mchezo mwingine katika kundi hlao la A, timu za Athletico Abidjan na Sporting Casablanca ya Morocco zikitoka sare ya 1-1.