Nyota wapya Azam FC waanza mazoezi

Beki mpya wa Azam FC, Colombia Yeison Fuentes, akifanya mazoezi yake ya kwanza na wachezaje wenzake

KANDANDA Nyota wapya Azam FC waanza mazoezi

Zahoro Mlanzi • 20:16 - 23.01.2024

Ni wachezaji wawili wa kimataifa kutoka Colombia na mwingine ni kutoka Sudani Kusini

Nyota wapya wa kikosi cha timu ya Azam FC, ambao wamewasajili katika dirisha dogo, tayari wamejiunga na timu hiyo kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mechi zilizosalia katika Ligi Kuu na michuano ya FA Cup.

Katika mazoezi yaliyofanyika chini ya Kocha, Yusuph Dado, Azam imetoa taarifa kuwa mlinzi wao mpya wa kati raia wa Colombia, Yeison Fuentes amejiunga na wenzie katika maandalizi ya kikosi chao.

"Tunayofuraha kumpokea kikosini mlinzi wetu mpya Fuentes katika mazoezi kwa mara ya kwanza akiwa na wenzake," imesomeka taarifa katika kurasa rasmi za mitandandao ya klabu hiyo.

Mlinzi huyo alijiunga na Azam kwenye dirisha lililopita la usajili akitokea kwenye Ligi ya Colombia akitokea timu ya Leones FC.

Huyo alikuwa ni mchezaji wa mwisho kwa Azam kutangazwa katika usajili wao.

Awali Azam waliwatangaza Franklin Navarro ambaye alicheza baadhi ya michezo katika Mapinduzi Cup, pia walimtambulisha mlinda lango wa El-Marrekh ya Sudan, Mohamed Mustapha ambaye walimsajili kwa mkopo wa miezi sita.

Wachezaji wote hao wapya ambao wamejiunga na timu wapo kambini wakiendelea kujifua kwa mazoezi makali chini ya kocha wao.

Azam inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na alama 31 ikifuatiwa na Yanga yenye alama 30 ila ipo nyuma kwa michezo miwili dhidi ya vinara hao.

Tags: